Ruka kwenda maudhui

Uasi wa Kisaikolojia

Wale wenye wamejitolea kusafiri inchi zote za dunia na makusudio ya kujifunza kwa kina jamii zote za wanadamu, wameweza kujionea wenyewe kwamba tabia ya hiki KIUMBE AKILI maskini inayoitwa kimakosa binadamu, ni ileile, iwe ni katika Ulaya ya zamani ama Afrika iliyochoka na utumwa mwingi, katika nchi takatifu za Vedas ama katika India ya Magharibi, katika Austria ama katika China.

Hii jambo la hakika, hii ukweli kubwa yenye kushangaza kila mutu mwenye kusoma, inaweza kuthibitishwa hasa kama msafiri anatembelea Mashule, Makoleji na Vyuo Vikuu.

Tumefika wakati wa uzalishaji kwa wingi. Sasa kila kitu kinazalishwa kwa mfululizo na kwa wingi kubwa. Mfululizo ya Ndege, Magari, Bidhaa za Anasa, nk., nk., nk.

Ijapokuwa inaonekana, kidogo ya ajabu, ni kweli kabisa kwamba Mashule za Ufundi, Vyuo Vikuu, nk pia zimekuwa viwanda akili vya uzalishaji kwa wingi.

Katika hii nyakati za uzalishaji kwa wingi lengo pekee katika maisha ni kupata usalama wa kiuchumi. Watu wanaogopa kila kitu na wanatafuta usalama.

Kufikiri kwa kujitegemea katika hii nyakati za uzalishaji kwa wingi, inakuwa karibu haiwezekani kwa sababu aina ya kisasa ya Elimu inategemea maslahi tu.

“Mganda Mpya” unaishi sawa sana na hii hali ya kawaida ya akili. Kama mutu anataka kuwa tofauti, kinyume na wengine, kila mutu anamshusha, kila mutu anamkosoa, anatengwa, anakataliwa kazi, nk.

Tamaa ya kupata pesa ya kuishi na kuburudika, uharaka wa kufikia mafanikio katika maisha, utafutaji wa usalama, kiuchumi, tamaa ya kununua vitu vingi vya kujionesha mbele ya wengine, nk., inasimamisha mawazo safi, ya asili na ya moja kwa moja.

Imeweza kuthibitishwa kabisa kwamba uoga unalemaza akili na unagumuisha moyo.

Katika hii nyakati za uoga mingi na utafutaji wa usalama, watu wanajificha katika mapango yao, katika mashimo yao, katika kona yao, katika mahali wanaamini wanaweza kuwa na usalama mwingi, matatizo kidogo na hawataki kutoka huko, wana uoga wa maisha, uoga wa matukio mapya, kwa uzoefu mpya, nk., nk., nk.

Hii yote ELIMU ya kisasa yenye KUJISIFIA inategemea uoga na utafutaji wa usalama, watu wanaogopa sana, wanaogopa hata kivuli chao wenyewe.

Watu, wana uoga wa kila kitu, wanaogopa kutoka katika kanuni za zamani zilizowekwa, kuwa tofauti na watu wengine, kufikiri katika njia ya mapinduzi, kuvunja na chuki zote za Jamii inayoharibika, nk.

Kwa bahati nzuri wanaishi katika dunia watu wachache wa kweli na wenye kuelewa, ambao kwa kweli wanataka kuchunguza kwa kina matatizo yote ya akili, lakini katika wengi wetu hata hamna roho ya kutokubaliana na uasi.

Kuna aina mbili za UASI ambazo zimekwisha kuainishwa vizuri. Ya Kwanza: Uasi wa Kisaikolojia wa vurugu. Ya Pili: Uasi wa Kisaikolojia wa kina wa AKILI.

Aina ya kwanza ya Uasi ni Mwitikiaji mhafidhina na wa kurudisha nyuma. Aina ya pili ya Uasi ni MAPIINDUZI.

Katika aina ya kwanza ya Uasi wa Kisaikolojia tunampata MTENGENEZAJI ambaye anashona nguo za zamani na anarekebisha kuta za majengo ya zamani ili yasianguke, aina ya kurudi nyuma, Mwanamapinduzi wa damu na pombe, kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi na mapinduzi ya Serikali, mutu wa bunduki begani, Dikteta ambaye anafurahia kuwapeleka ukutani wale wote wasiokubali ubunifu wake, nadharia zake.

Katika aina ya pili ya Uasi wa Kisaikolojia tunampata BUDDHA, YESU, HERMES, mgeuzi, MUASI MWENYE AKILI, MWENYE KUONA, mabingwa WAKUBWA wa MAPIINDUZI YA FAHAMU, nk., nk., nk.

Wale ambao wanajielimisha tu kwa makusudio ya ajabu ya kupanda nafasi nzuri ndani ya mzinga wa urasimu, kupanda, kupanda juu ya ngazi, kujionesha, nk., hawana kina cha kweli, ni Wapumbavu kwa asili, wasio na kina, matupu, asilimia mia wahuni.

Imekwisha kuthibitishwa hadi kutosheka kwamba wakati katika binadamu hakuna UUNGANISHO wa kweli wa mawazo na hisia, ingawa tumepokea elimu kubwa, maisha yanakuwa hayajakamilika, yanapingana, yanachosha na yanateswa na hofu nyingi za kila aina.

Bila shaka yoyote na bila kuogopa kukosea, tunaweza kusema kwa nguvu kwamba bila elimu KAMILI, maisha yanakuwa ya hatari, hayana maana na yana madhara.

KIUMBE AKILI kina EGO YA NDANI iliyo na bahati mbaya na VITU mbalimbali ambavyo vinajizidisha nguvu na ELIMU POTOFU.

MIMI MWENYE KUJUMUISHA ambao kila mmoja wetu tunabeba ndani, ndio sababu ya msingi ya matatizo na mizozo yetu yote.

ELIMU YA MSINGI inapaswa kufundisha vizazi vipya DIDAKTIKI yetu ya Kisaikolojia kwa AJILI YA KUVUNJA MIWILI.

Ni kwa kuvunja tu vitu mbalimbali ambavyo kwa ujumla vinaunda Ego (MIMI) tunaweza kuanzisha ndani yetu kituo cha kudumu cha ufahamu wa mtu binafsi, ndipo tutakuwa WAKAMILIFU.

Wakati MIMI MWENYE KUJUMUISHA iko ndani ya kila mmoja wetu, hatutaumiza tu maisha wenyewe lakini pia tutawaumiza wengine.

Inafaa nini kusoma sheria na kuwa mawakili, kama tunaendeleza kesi? Inafaa nini kukusanya katika akili zetu maarifa mengi, kama tunaendelea kuchanganyikiwa? Ni nini faida ya ujuzi wa kiufundi na wa viwandani kama tunatumia kwa ajili ya uharibifu wa wenzetu?

Hakuna maana ya kujifunza, kuhudhuria madarasa, kusoma, kama katika mchakato wa maisha ya kila siku tunaharibiana kwa huzuni.

Lengo la elimu haipaswi kuwa tu kuzalisha kila mwaka watafuta kazi wapya, aina mpya ya wahuni, watu wapya wasiojua hata kuheshimu Dini ya jirani, nk.

Lengo la kweli la ELIMU YA MSINGI inapaswa kuwa kuunda wanaume na wanawake wa kweli WENYE KUUNGANISHWA na kwa hivyo wanaojitambua na wenye akili.

Kwa bahati mbaya Walimu na Walimu wa Kike wa Mashule, Makoleji na Vyuo Vikuu, wote wanafikiria, isipokuwa kuamsha AKILI KAMILI ya WAFUNZI.

Mutu yeyote anaweza kutamani na kupata majina, mapambo, diploma na hata kuwa na ufanisi sana katika uwanja wa mitambo wa maisha, lakini hii haimaanishi kuwa MWENYE AKILI.

AKILI haiwezi kuwa utendaji wa mitambo tu, AKILI haiwezi kuwa matokeo ya habari rahisi ya vitabu, AKILI sio uwezo wa kuguswa moja kwa moja na maneno ya kung’aa kwa changamoto yoyote. AKILI sio mazungumzo tu ya kumbukumbu. AKILI ni uwezo wa kupokea moja kwa moja KIINI, HALISI, kile kilicho kweli.

ELIMU YA MSINGI ni sayansi ambayo inaturuhusu kuamsha uwezo huu ndani yetu na kwa wengine.

ELIMU YA MSINGI inasaidia kila MTU kugundua THAMANI za kweli zinazojitokeza kama matokeo ya uchunguzi wa kina na UELEWA KAMILI WA MWENYEWE.

Wakati hakuna ndani yetu KUJIJUA, basi KUJIELEZA inakuwa KUJITHIBITISHA KWA UBINAFI na KWA UHARIBIFU.

ELIMU YA MSINGI inajali tu kuamsha katika kila mutu UWEZO wa kujielewa mwenyewe katika nyanja zote za akili na sio tu kujitoa kwa kuridhika kwa KUJIELEZA potofu kwa MIMI MWENYE KUJUMUISHA.